Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Akizungumza na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ali-Akbar Ajāq-Nezhād, jioni ya Jumanne katika mkusanyiko wa kiapo cha utii cha umma kwa Wilaya na hafla ya kuhuisha kiapo cha utii kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, iliyofanyika kwa mahudhurio makubwa ya wapenda na wanaomsubiri Imam wa Zama (a.j) katika eneo takatifu la Msikiti wa Jamkaran, alisema: kufuatia matukio machungu yaliyotokea katika siku za hivi karibuni kwa mchango wa Marekani na utawala wa Kizayuni, taifa la Kiislamu la Iran kwa uwepo wake mpana katika uwanja, liliweza kuvuruga njama hizo, na maadui ambao hawakuweza kuvumilia kushindwa huku, wakafanya dharau na matusi dhidi ya matukufu ya dini, taifa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Kiapo cha umma kwa Wilaya katika Msikiti Mtakatifu wa Jamkaran
Akiendelea kusema kwamba ushindi wa taifa la Iran umetokana na uongozi wa busara na hekima wa Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei, aliongeza: ushindi huu ulikuwa ukurasa mwingine wa dhahabu katika historia ya mapambano ya kupinga ubeberu katika taifa la Iran, ambao kwa msaada wa nusra ya Mwenyezi Mungu na kutimia kwa ahadi ya Mola juu ya kushinda kwa haki dhidi ya batili, ulipatikana.
Kwa mujibu wa msimamizi wa Msikiti Mtakatifu wa Jamkaran, rais mwenye kiburi wa Marekani, aliposhuhudia tarehe 12 January mahudhurio ya mamilioni ya wananchi wa Iran katika kulaani ghasia, na kuona kushindwa kwa juhudi zake za miezi kadhaa za kuunda fitna, kama madikteta wa historia, alianza kutupa maneno machafu, matusi na vitisho, na akaweka wazi chuki yake kutokana na kushindwa mfululizo mbele ya uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Akirejea kutimia kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu madhalimu, alisema: usiku wa leo tumekusanyika katika Msikiti Mtakatifu wa Jamkaran ili kutangaza uungaji mkono na kiapo chetu cha utii kwa Naibu wa Imam wa Zama (a.j), na taifa la Iran pia linatangaza kwamba kama lilivyovunja mgongo wa fitna, halitakaa kimya mbele ya wafitnishaji wa kigeni.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ajāq-Nezhād, akisisitiza kwamba kudharau hadhi takatifu ya uongozi hakutapita bila jibu, aliongeza: Umma wa Kiislamu, taifa la Iran na watu huru duniani hawatawaacha wanaodharau nafasi ya Wilaya, na wanawachukulia kama mhalifu anayepaswa kufuatiliwa.
Alibainisha: leo Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa niaba ya umma wa Kiislamu, amesimama dhidi ya dhulma za madhalimu, na kwa ujasiri analinda heshima ya dini, mamlaka ya Iran na umoja wa ardhi ya nchi, na sisi pia tutatetea Wilaya na Mapinduzi ya Kiislamu hadi tone la mwisho la damu yetu.
Msimamizi wa Msikiti Mtakatifu wa Jamkaran pia alisisitiza juu ya nukta hii ya msingi kwamba, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni mstari mwekundu wa ulimwengu wa Kiislamu, na aina yoyote ya shambulio au uvunjaji wa heshima dhidi ya Wilaya na fiqhi ya Kiislamu itakabiliwa na radi amali ya pamoja katoka katika umma wa Kiislamu, na maadui wanapaswa kusubiri madhara yake makubwa.
Mwisho, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ajāq-Nezhād, huku akitoa shukrani kwa uwepo wa kishujaa wa wananchi katika maandamano ya Siku ya Mwenyezi Mungu ya 12 January, alivishukuru vikosi vya usalama, kijeshi na vya Basij, pamoja na maafisa na viongozi wa mihimili mitatu ya dola, na akataka kuchukuliwa hatua za kijihadi na za kitaalamu kwa ajili ya kutatua matatizo ya kiuchumi na kuboresha hali ya maisha ya tabaka mbalimbali za wananchi.
Maoni yako